Mshindi wa shindano la Big Brother Africa 2014, Hotshots Idris Sultan, amedai kwa sasa hana mpenzi.
Akiongea Bongo5 wiki hii, Idris amedai misukosuko aliyoipata baada ya kuweka wazi maisha ya mahusiano yake na malkia wa filamu, Wema Sepetu, imetosha.
“Mimi niko single, na siwezi kuweka wazi mahusiano yangu kwa sababu fulani kaweka wazi mahusiano yake,” alisema Idris Sultan.
Aliongeza, “Mahusiano yako ya mapenzi ukiyafanya kila mtu ajue inakuwa ni tatizo, nikipata mpenzi na nikiona kuna umuhimu kwa mashabiki wangu kujua nitafanya, lakini kwa sasa hivi siwezi kufanya hivyo,”
Kwa sasa mchekeshaji huyo ni balazi wa amani nchini Tanzania.
-Bongo5