Kiongozi wa kanisa katoliki anayewasaidia raia wa Malta amejiuzulu kufuatia mgogoro na Vatican kuhusu mpango wa kusambaza mipira ya kondomu kulingana na kanisa hilo.
Mathew Festing mwenye umri wa miaka 67 alijiuzulu baada ya papa Francis kumtaka kufanya hivyo katika mkutano siku ya Alhamisi. Hatua hiyo inafuatia ufichuzi kwamba tawi la hisani la kanisa hilo huko Malta lilisambaza maelfu ya mipira ya kondomu katika taifa la Myanmar.
Kanisa katoliki linakataza utumizi wa mipira ya kondomu. Papa Francis alimtaka ajiuzulu na alikubali. Tawi hilo la Malta lina uwezo mwingi kama ule wa taifa zima. Hutoa pasipoti, stampu na leseni na pia lina uhusiano wa kidiplomasia na mataifa 106 ,ikiwemo Vatican.