Msanii wa muziki singeli Man Fongo amesema anakumbuka alipoanzia muziki wake kwa kuimba nyimbo za vigodoro na ipo siku atarudi uswahilini kuwaimbia mashabiki zake.
Akiongea kupitia eNewz amesema singeli ni muziki wa watu masikini na watu wa hali ya chini na umetokea uswahilini kwani mwanzo alipokuwa akiimba alikuwa analipwa hela ndogo hadi elfu ishirini pia kulikuwa na misukosuko mingi ikiwemo kushikiwa mapanga na kuwekewa mawe aimbe hadi asubuhi.
Hata hivyo Man Fongo anasema zamani alipokuwa anaimba muziki wa singeli alikuwa anakuwa na watu mbalimbali wa uswahilini waliokuwa wakimfuata nyuma hali iliyopelekea mpaka watu kuhisi kwamba ni vijana wa panya road japo walikuwa mashabiki