Jengo la ghorofa tatu lilokuwa katika ukarabati katika Mjimkongwe wa Zanzibar limeporomoka na kuua mtu moja na mwengine kujeruhiwa vibaya.
Jengo hilo la ghorofa tatu ambalo liko katika mtaa wa Mjimkongwe lilianguka wakati mafundi wawili wakiwa wako kazini na ghafla ukuta wa mbele ukaporomoka na kuwatupa barabarani ambapo moja ya fundi huyo, aliokolowa na wananchi na kumpeleka hospitali kuu ya Mnazimoja huku hali yake ikiendelea kuwa nzuri ,lakni pamoja na jitihada za kikosi cha ziamamto na wananchi kujaribu kumuokoa fundi mwingine hazikufanikiwa na fundi huyo alifariki baada ya kufukuliwa na kikosi hicho na maiti yake kupelekwa hospitali kuu ya Mnazimoja kwa uchunguzi kabla ya familia kukabidhiwa kwaajili ya maziko ambapo kamanda wa polisi Mjinimagharibi Kamishna Msaidizi mwanadamizi wa polisi Hassan Nasser alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Wakizumgumza mashuhuda walioshudia jengo hilo likiporomoka ambalo ni mali yawakfu na mali amana wamesema ilikuwa ni mshutko mkubwa ambao uliwashtua wananchi wa hapo lakini bahati nzuri hapakuwepo na wapita njia wakati udongo na mawe yakiporomoka ingawa ni pikipiki moja iliyokuwa imeegemezwa ilifunikwa huku injinia wa mamlaka ya Mjimkongwe Mussa Awesu Bakari amesema ujenzi wa jengo hilo ulikuwa unafanyika kwa mujibu wa sheria na taratibu zote za mamlaka ya Mjimkongwe.