SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 15 Desemba 2016

T media news

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 103 & 104 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA

Nikamvuta na kumuingiza chooni, mikamuonyesha bomu lilipo, Sote tukajikuta tunashangaa kutokana bomu hilo limebakisha sekunde hamsini na tisa, kabla halijalipuka na sote hapa hatujui jinsi ya kulitegua, na muhudumu akaanza kulia, akijaribu kunikumbatia kwani mwisho wetu umefika.

ENDELEA

"Una chochote cha kukatia"

Nilizungumza huku nikimtoa muhudumu huyu, mwilini mwangu, kwani kukumbatiana kwetu sio suhulisho la bomu hili kuacha kuacha kulipuka. Hakunijibu zaidi ya kubabaika, kwa mawenge yaliyo mchanganya kupita maelezo. Akaanza kujipapasa huku mwili mzima ukimtetemeka kwa woga, akatoa, kikatia kucha(Nail cutter), akaitupa chini huku akiendelea kuikagua mifuko ya nguo zake alizo zivaa. Kwa haraka nikaokota kikatia kucha, nikapiga magoti chini, huku nikiwa ninajiamini kwa lile ninalo kwenda kulifanya.

   Sekunde za bomu hili, zikazidi kurudi nyuma, huku zikiwa zimebakia sekunde thelathini na mbili kabla halijalipuka. Nikaanza kuzichambua nyaya nyingi ndogondogo zipatazo ushirini, zikiwa na rangi tofauti tofauti.

"Ishirini na tano"

Muhudumu aliniambia, huku macho yake akiwa ameyatumbulia kwenye bomu, linalo zionyesha sekunde hizo, zinavyo rudi nyuma.

"Mungu wangu"

Nilizungumza huku nikizidi kuchanganyikiwa, kwani sikujua ni waya upi unanipasa kuukata, ili kulizuia bomu hili kuto kulipuka.

"Kumi na tano"

Nikashika nyaya moja nyekundu na kuikata, chakushangaza, bomu likaendelea kurudisha sekunde zake nyuma.

"Nane"

Nikazidi kuchanganyikiwa, na kukata wanya mweusi, hali ikawa ni ile ile.

"Tano"

Mikono yote, ikazidi kutetemeka hadi nikaangusha kikatia kucha, nikakiokota kwa haraka, hata kukaa mkononi vizuri, nkawa ninashindwa kukishika.

"Tatu"

Nikamuona muhudumu, akipiga ishara ya msalaba akiashiria mwisho wetu ndio unakaribia, nikashika waya wa rangi ya kijani, sekunde ikawa imebaki moja, nami nikawa nimeukata. Sekunde hiyo ikasimama hapo hapo na bomu kuzima. Nikashusha pumzi nyingi, huku mwili wangu wote ukiwa umesha vuja jasho lakutosha hadi shati nililo livaa, likawa limelowana kabisa. Kumtazama muhudumu nikamkuta akiwa ameyafumba macho yake huku jasho likimwagika shingoni nwake.

"Tumefanikiwa"

Nilizungumza kwa sauti ya unyonge huku nikimtazama usoni muhudumu, akayafumbua macho yake taratibu, huku akihema. Akalitazama bomu nililo lichomoa na kulishika, akabaki akiwa ameduwaa. Akanishika mkono taratibu na kuninyanyua, akanikumbatia huku akilia kwa furaha.

"Asante Mungu, kweli wewe ni mwema. Hakuna kama wewe"

Alizungumza huku akiendelea kulia, nakunifanya na mimi machozi kunimwagika kwani sikutarajia kama nitaweza kufanikiwa kulitegua bomu hili, taratibu akaniachia, huku akijifuta machozi usoni

"Unaitwa nani?"

"Eddy, Eddy Godwin"

"Am Tasiana, from Arusha Tanzania"(Mimi ni Tasiana natokea Arusha Tanzania)

"Mimi pia natokea Tanzania, ila A leve nilisoma Arusha"

"Waooo, nashukuru kukufahamu"

Tasiana akanikumbatia kwa mara ya pili, akawasiliana na marubani wa ndege hii, kupitia kijisimu kidogo wanacho kitumia kuwasiliana, wakamuomba tuelekee kwenye chumba walipo, tukiwa na bomu hilo, ila tuhakikishe hakuna abiria atakaye liona, ili kuto hatarisha amani ya walio wengi.

Tasiana akachukua mfuko mtupu, mweusi. Akaliweka bomu, nikaongozana naye hadi chumba cha marubani. Tukawaelezea hali halisi juu ya tukio zima na jinsi mchungaji Frank, alivyo nipa vitisho nikiwa ninapishana naye kwenye mlango wa chooni.

"Hakuna aliye toka ndani ya ndege, ngoja tukifika Afrika kusini, tutafanya upelelezi kabla watu hawaja ruhusiwa kushuka kwenye ndege"

Rubani mmoja alizungumza huku akilitazama tazama bomu hilo nililo mpatia.

"Ukimuona si utamkumbuka?"

"Ndio, nilikuwa nimekaa naye ila simuoni kwenye siti yetu"

"Ulikaa siti gani?"

Nikamtajia rubani, huyo herufi ya siti niliyo kuwa nimekaa, akatazama mkanda mzima, kwenye kiji tv chao kidogo unao rekodiwa na kamera zilizo tegwa kila kona ya ndege. Tukamuona mzee huyo akiingia kwenye moja ya chumba walicho dai ni stoo, chenye gazi za kushukia chini, kunapo hifadhiwa mizigo mikubwa mikubwa.

"Ngoja nimfwate"

Nilizungunza kwa kujiamini, huku nikiwatazama marubani hawa wapatao wanne, huku wawili wakiwa niwasaidizi.

"Itaweza kumkamata?"

"Nitahakiksha nalifanikisha hilo"

Wakanitazama machoni, mkuu wao akanipa ruhusa.

"Tuongozane"

Tasiana aliomba tuongozane pamoja.

"Wewe baki, ngoja nikajaribu kulifanya na hili kama nitafanikiwa"

"Tafadhali twende pamoja"

Tasiana aling'ang'ania kwenda, ikanibidi nimkubalie tu. Tukaongozana hadi kwenye chumba hicho, pasipo wasafiri wezangu kuelewa kitu gani kinacho endelea, hakikuwa chumba kikubwa sana, kwani kina ngazi zakushuka chini kulipo na mizigo mikubwa. Tukafanikiwa kushuka chini, kwa wingi wa mizigo iliyo fungwa kwenye mifurushi mikubwa, ilitufanya tubaki tukiwa tumesimana na kuduwaa.

"Atakuwa wapi?"

Tasiana aliniuliza kwa sauti ya chini, huku tukiendea kupepesa pepesa macho yetu kila kona ya eneo hili lilolo kubwa.

"Nifwate nyuma na kuwa mkimya"

Tukaanza kupita kwenye vinjia, vilivyo tenganishwa kwa maburungutu makubwa ya mizigo. Nikaanza kupata wasiwasi, baada ya kukuta shati alilo kua amelivaa mzee yule, likiwa chini. Tasiana akataka kuliokota ila nikamzuia asifanye hivyo.

"Kwa nini nisiliokote?"

Nikatingisha kichwa nikimuashiria Tasiana asifanye chochote dhidi ya shati hilo.Tukalipita, hatua kumi mbele, tukakuta suruali aliyo kuwa ameivaa.

Kwa kutumia mguu nikaisogeza kuitazama kama kuna kitu kimefunikwa, ila hatukuona kitu.

Arufu ya moshi wa sigara, ukaanza kuingia kwenye pua zetu, ulitokea upande wa pili wa sehemu ilipo mizigo hiyo. Tukapiga hatua za tahadhari hadi sehemu inapo tokea harufu ya moshi huo wa sigara, tukakuta kipande cha sigara kikiwa chini, kikiendelea kuteketea taratibu.