SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 15 Desemba 2016

T media news

KINANA AZINDUA JENGO LA KITEGAUCHUMI LA CCM, UPANGA JIJINI DAR ES SALAAM, LEO

Jengo la kisasa la Kitegauchumi la Chama Cha Mapinduzi (CCM), lilipo Upanga jijini Dar es Salaam, lililozinduliwa leo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana. 

Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Anna Abdallah, ujenzi wa jengo umegharimu sh. Bilioni saba.Mama Anna Abdallah, amesema, jengo hilo limejengwa kwa hali ya juu na limewekwa kila kitu ikiwemo zamani.

"Mpangaji anapotaka kuingia katika nyumba hii, yeye anachopaswa kufanya ni kuja na chakula na nguo tu, halazimiki kuingia na samani yoyote hata TV anaikuta ipo sebuleni", Alisema, Mama Anna.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua jengo la kisasa la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mama Zakia Megji na Mama Anna Abdallah.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua rasmi jengo hilo. Kushoto kwake ni Mama Anna Abdallah na kulia kwake ni Mama Zakia Meghji.
Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Meghji akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la Kisasa la Kitegauchumi la CCM, lilipo Upanga jijini Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya waalikwa wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo la kisasa la kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo. 


Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa mali za CCM, Mama Anna Abdallah, akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la Kisasa la Kitegauchumi la CCM, lilipo Upanga jijini Dar es Salaam, leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza kabla ya kuzindua jengo la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia baadhi ya wanachama wa CCM wakati akienda kuzindua jengo la Kitegauchumi la CCM, lililopo Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mama Zakia Meghji

Katibu Mkuu wa CCM, Andulrahman Kinana akienda kukagua ndani ya jengo
Kinana akitazama ukumbi wa mikutano katika jengo hilo
Kinana akisalimiana na mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa mali za CCM wakati akikagua jengo.

Samani ndani ya jengo
🔻


jikoni




Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na baadhi ya viongozi kabla ya kuondoka baada ya kuzindua rasmi jengo la kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO