SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 11 Septemba 2016

T media news

Wapigaji uwanja wa Taifa sasa basi

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye amezindua mfumo mpya wa tiketi wa kielektroniki (Electronic Ticketing System) kwenye uwanja wa taifa ambao utakuwa ukidhibiti mapato.

Mfumo huo ambao unasimamiwa na kampuni ya BCG pamoja na Selcom tayari umefungwa kwenye mageti yote ya kuingilia na upo tayari kwa matumizi.

Jinsi mfumo utakavyofanya kazi

Kuna kadi maalum ambazo zitatolewa bure na Selcom ambazo zitaunganishwa moja kwa moja na namba ya simu ya mtumiaji wakati wa usajili.

Watazamaji watakuwa wakinunua tiketi kwa mawakala wa Selcom wanaopatikana nchi nzima au kupitia simu zao za viganjani.

Baada ya kununua tiketi, mtazamaji atapokea ujumbe mfupi wa maandishi utakaompa malekezo atakaa jukaa gani kulingana na bei ya tiketi yake.

Mtazamaji atakapofika uwanjani ata-tap kadi yake kwenye mashine maalumu ambayo itaruhusu mlango kufunguka kisha ataingia ndani.

Mgao wa pesa utakuwa ukifanyika kwa njia ya ki-electronic bila kugusa fedha (cash). Wadau wote wanaohusika katika mgao huo kwa mfano TFF, uwanja, serikali, na wengine watapata fedha zao pindi tu tiketi inaponunuliwa.

Faida ya kutumia electronic tickets

Ni rahisi kujua idadi ya watu walioingia uwanjani kwasababu hakuna mtu yeyote atakaeweza kuingia uwanjani bila tiketi.

Usalama mkubwa wa pesa kwasababu hazitakuwa mikononi mwa watu kwahiyo haitahitaji ulinzi wa ziada. Serikali itapata kodi yake kwa uhakika kulingana na mapato yaliyokusanywa.

Inatajwa kuwa, mfumo huo unaweza kutumiwa pia katika uwanja wa Uhuru kupitia mageti yaliyopo Kusini mwa uwanja wa Taifa.