SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 8 Septemba 2016

T media news

SHILOLE KIUNO AFUNGUKA HAYA -: SIWEZI KUTEMBEA NA MZEE, MAISHA YANGU

“Badgirl Shishi himself” ni baadhi ya maneno ambayo nilimnukuu mwanadada Shilole alipokuwa akifanyi interview na kipindi kimoja cha Clouds Tv.Sasa hiyo siyo kesi, kesi ni maneno ambayo yanazungumzwa mtaani kumuhusu mwanadada huyo kwamba yeye pigo zake ni dogodogo na hapendelei kuwa na wanaume wa rika lake.Mapovu yamemtoka mwanadada huyo jana alipokuwa akihojiwa na E-News ya EATV na kudai kwamba mashabiki zake hawatakiwi kuya fuatilia maisha ya Zuwena bali wanatakiwa ku-deal na maisha ya Shilole. Akiwa na maana kwamba yeye akiwa nyumbani kwake ni Zuwena na sio Shilole, kwahiyo maisha yakwake binafsi hayawahusu mashabiki zake kwahiyo wampe nafasi kidogo.
“Mimi naangalia upendo wangu uko wapi, nikisema nifuate sana mashabiki wanachotaka wenyewe wanataka niwe na mzee, sasa me naanzaje kuwa na mzee? Me nahangaika kutafuta pesa halafu nihangaike tena na wazee? Lazma niwe na kijana mwenzangu ili anipetipeti.” Aliongeza mwanadada Shilole.