SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 6 Septemba 2016

T media news

PADRI MAPUNDA AKOSOLEWA VIKALI BAADA KUMSHUKIA RAIS MAGUFULI

VIONGOZI WA DINI MSITUMIKE VIBAYA MTABOMOA TAIFA LETU.
Baada ya kusoma gazeti la Tanzania Daima, Toleo NA.4284 la September 5,2016 ninaomba nimkosoe vikali Baba Padri Baptiste Mapunda kwa alichokiongea kanisani akiendesha misa takatifu tarehe 4,September 2016 katika kanisa katoliki la Manzese Dar es salaam.

Baba padri Mapunda aliongea Maneno makali na yasiyofanyiwa utafiti wa kina, na pengine maneno yasiostahiri kusemwa katika mahubiri maana yanaweza kubomoa Taifa letu na kupandikiza chuki miongoni mwa wahumini husika na kuweza kuchukia serikali yao, mfano,padri Mapunda alisema "Rais Magufuli awe na busara na kufuata mwenendo wa Nabii Suleiman....."tafasili yake ni kwamba Mh,Rais wetu hana busara na kama hana busara sisi wote Tanzania tuliomchagua hatuna busara na hii dhahiri kuwa baba Padri anataka tumchukie mh,Rais kwa kisingizio cha kwamba hana busara.

Padri Mapunda anaenda mbali na kusema nina nukuu "wananchi wanalalamika kuongezeka kwa ugumu wa maisha kwa kutokuwa na fedha na kukosekana kwa demokrasia" anamalizia kwa kuhalalisha uongo huu kuwa ukweli kwa kusema nanukuu "Mungu yupo na anayaona mateso ya watanzania".

Ndugu msomaji wangu kama utatafakali hizo nukuu hizo hapo juu utagundua pengine huyu mh,Baba Padri alitakiwa kuwa mwanasiasa ila kakosea kusomea upadri maana anasahau hata maandiko ya Mungu yanayosema "asiyefanya kazi na asile" hakika kuna watanzania wanalalamika kutokuwa na fedha Wakati wakishinda vijiweni, wakishinda wanacheza pulu na wengine hushinda vilabuni na hakuna serikali yeyote inayoweza kumletea mtu pesa mfukoni bila kufanya kazi.

Kuhusu swala la demokrasia, ilipaswa Baba padri useme ni demokrasia ipi wewe unataka na watanzania umesikia wanataka hawana,na mh,Rais kaibana? Je ya kuuza madawa ya kulevya?,ya kuua Tembo?, au ya ufisadi maofsini?. maana haya ndo mh,Magufuli hataki kuyaona na hakika amefanikiwa kuyapiga marufuku nami namuomba aendelee kuyazuia.

Jambo lingine padri Mapunda anasema mh,Magufuli akubali kukosolewa kama mwenyezi Mungu alivyokuwa akikosolewa na Nabii Mussa, nanukuu Maneno yake,naomba nimkumbushe Baba padri kuwa kukosoa ni sahihi wala mh,Magufuli hajasema hapendi kukosolewa lakini siyo kila jambo lazima ukosoe pengine unaweza kukosoa na kisichostahili kwa maslahi ya umma.

Hata Nabii Mussa mwenyewe kitendo chake cha kumkosoa Mungu kwa kila jambo kulimsababishia mauti, akiwa anatoka Misri kuwakomboa wana wa Israel kuelekea katika nchi ya ahadi, na akafa kabla ya kuiona nchi ya ahadi. Kwahiyo sio wote wanaomkosoa Mh,Rais wako sahihi,wengine ni kutaka kujiona jeuri zaidi ya Mh,Rais kwakutofuata sheria,maelekezo na utawala wa sheria kama Nabii Mussa huyo uliyemsema alivyokataa kufuata maelekezo ya mwenyezi Mungu na kuishia pabaya.

Lakini kuna maswali ya kujiuliza hapa kabla ya kuendelea;

1, Je huyu mwandishi wa habari nani aliyemuita kanisani kuja kuchukua hii habari?
2, Na kama hajaitwa yeye alijuaje kuwa Baba padri anaenda kumkosoa mh,Magufuli na yeye kuja kuandika?

3, Na kama kaitwa nani aliyemlipa hiyo pesa? maana kwa uzoefu waandishi wa habari wamekuwa wakilipwa posho pindi wanapoitwa.

4, Je baba padri yeye kama kiongozi wa dini ameomba nafasi ya kuonana na Mh,Magufuli ili amshauri amekosa?

5,Mpasuko aliodai uko nchini hakika una chanzo chake na Chanzo ni Chadema kutangaza maandamano ya nchi nzima, swali Je Chadema ilipotangaza maandamano Padri Mapunda aliwaita na kuwakanya pamoja na kuwapa ushauri? au ndo kutaka umaarufu? Au kapewa pesa na Chadema kuja kuanza chokochoko?

Baada ya kujiuliza maswali hayo utagundua kuna kitu kimejificha katikati, kwasababu haiwezekani Padri Mapunda ainuke na kuhukumu kuwa Mh,Rais ni mbaya na hana busara kabla ya kukaa na hizi pande mbili na kuzihoji, ikumbukwe kuwa chombo pekee cha kuhukumu kuwa nani mbaya kati ya Mh,Magufuli na Chadema ni Mahakama na baada ya kusikiliza pande zote kwakufuata katiba ya nchi ibara ya 13.

Hata mwenyezi Mungu kabla ya kumuhukumu Adam na Hawa aliwasikiliza wote baadae ndo katoa adhabu mbili tofauti; Hawa akaambiwa atazaa kwa uchungu, na Adamu kaambiwa atakula kwa jacho.

Mwisho nimuombe Baba padri Mapunda aige mfano wa Bwana yetu Yesu kristu mpatanishi aliyekuwa aegemei upande wowote katika kuhubiri injiri na wewe baba padri uwe mpatanishi, usiwapotoshe wana kondoo wa Mungu uliyopewa kuwafundisha kwa kuwachochea uhasama dhidi ya serikali yao.

Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema akunyooshee mkono wake wa kuume ewe padri Mapunda upate kuhubiri neno lake na sio siasa.
Imeandaliwa na mhumini wako,
MWITA NYARUKURURU
mwitanyarukururu@gmail.com

Source:Jamii Forums