SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 10 Septemba 2016

T media news

NI KUFA AMA KUPONA MANCHESTER UNITED VS MANCHESTER CITY LEO


Manchester United na Manchester City leo wana shughuli pevu katika Uwanja wa Old Trafford katika mchezo wa Ligi Kuu England utakachezwa 8:30 kwa majira ya Afrika Mashariki.

Hii ni vita ya makocha wawili ambao ni mahasimu wa muda mrefu Jose Mourinho na Pep Guardiola, ambapo kwa mara ya kwanza wanakutana katika historia ya soka la England baada ya kuwahi kukutana wakiwa La Liga kwenye vilabu vya Real Madrid na Barcelona.

Kwa upande wa Manchester United, wachezaji wao Luke Shaw na Henrikh Mkhitaryan wamepona majeraha yao, hivyo wanaweza kujumuishwa kwenye mchezo wa leo.

Antonio Valencia pia takuwepo baada ya kutoka kuitumikia timu yake ya taifa na kuondoa hofu kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Manchester City kwa upande wao, mshambulizi wa Sergio Aguero hatakuwepo kutokana na kutumikia adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu, Bacary Sagna anaweza kuanza baada ya kupona majeraha yake ya maumivu ya misuli ya paja.

Leroy Sane na Ilkay Gundogan wako fiti kabisa tayari kwa mchezo wa leo na wanaweza kupewa nafasi ya kuanza kwa mara ua kwanza kwenye ligi, vivyo hivyo kwa upande wa kipa Claudio Bravo.

Nahodha Vincent Kompany amepona na jana amefanya mazoezi kamili na wenziwe baada ya kukaa muda mrefu akiuguza majeraha ya paja, lakini leo hatakuwepo kwenye kikosi.

Kauli za mameneja wa timu zote mbili

Jose Mourinho juu ya kukosekana kwa mshambulizi wa City Sergio Aguero: “Ni vigumu zaidi kwetu. Inaonekana kutakuwa na hali ngumu kwenye mchezo wa leo, lakini bila ya Aguero ni vigumu zaidi.

“Aguero akiwepo, tunajua namna gani hucheza. Tunakuwa tunafahamu vizuri mfumo wao, namna wanavyocheza na hakuna shaka juu ya hilo.

“Wana options nyingi sana mabazo kwetu ilibidi tufanyie mazoezi sana, twende hatua kwa hatua, kuangalia kila namna ya kukabiliana nao ili kuzuia sintofahamu katika mchezo.”

Pep Guardiola: “Ngoja kwanza nicheze huu mchezo wa derby na baada ya hapo naweza kutoa tathmini ya kuangalia kama kuna ufanano na ila ya Hispania na Ujerumani. Kwa upande wa vyombo vya habari sijaona utofauti na Uhispania.

“Nimeona michezo minne rasmi ambayo United wamecheza na kwenye kila mchezo wamekuwa wakicheza vizuri zaidi. Kama ilivyo kwetu.

“Tuna kazi kubwa ya kuwadhibiti kwenye mipira ya juu, ni warefu kuliko sisi. Ni timu ya kiwango cha juu sana kama ambavyo miaka yote imekuwa.”
Head-to-head

City wanaingia uwanjani wakitafuta ushindi wa 50 katika mechi za mashindano kwenye Manchester derby (wameshinda mara 49, droo 51, kufungwa mara 71).Baada ya kupoteza michezo minne mfululilizo ya derby, Manchester United sasa hawajafungwa na City kwenye michezo minne (ushindi mara 2, droo mara 1). walipata clean sheets kwenye michezo yote waliyokutana msimu uliopita.United wamepoteza michezo mitatu kati ya mitano ya lligi dhidi ya Man City kwenye Uwanja wa Old Trafford (wameshinda mara 1, sare 1).Jose Mourinho ameshinda michezo mitatu ya ushindani kati ya 16 aliyokutana na Pep Guardiola (droo 6, amepoteza mara 7), ukiwemo ule wa ligi alioshinda dhidi ya Barca mwaka 2012 akiwa Real Madrid.