Baada ya kusababisha penati ya dakika za mwisho iliyopelekea kupoteza mchezo wao dhidi ya Arsenal kwa mabao 2-1, nahodha wa Southampton Jose Fonte ameonekana kusikitishwa na hali hiyo na kuamua kuomba radhi kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Beki huyo ambaye alijiunga na Southampton mwaka 2010, ameonesha kusikitishwa pia na uamuzi wa refarii akiamini kwamba haikuwa penati halali kwani yeye na Giroud wote walikuwa wakiwania mpira.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Fonte ameandika ujumbe mzito kwenda kwa mashabiki wote wa Southampton kuelezea hisia zake juu ya kile kilichotokea uwanjani.
Fonte, ambaye alikaribia kujiunga na Manchester United kwenye dirisha la usajili majira ya kiangazi lililofungwa hivi karibuni ameandika hivi:
“Just want to say thank you for the support and also for every fan that came to the game today!No one more then me feels hard done by and disappointed,you can feel the same but not more then me!When Giroud asks me who gave the penalty away that says it all,if you haven’t watched the game and come to criticise please save me that! We will keep our heads up and eager to turn this bad fortune around. Once again I appreciate the love. #wemarchon”.
Kwa Kiswahili
Ningependa kuwashukuru kwa mashabiki wote kwa kuja kutusapoti kwenye mchezo wa leo (jana)! Sidhani kama kuna mtu anayejisikia vibaya kutokana na matokeo haya zaidi yangu, inawezekana wote mna majonzi lakini si zaidi yangu! Kitendo cha Giroud kushangaa maamuzi yale yale ya penati na kuniuliza nani alisababisha penati kinadhihirisha kila kitu, kama haukuangalia mchezo na ukaja kukosoa, tafadhali amini hivyo! Tutajitahidi kupambana kadri ya uwezo wetu ili kupata matokea mazuri na kujiweka katika nafasi nzuri. Kwa mara nyingine tena nafurahishwa sana na mapenzi yenu ya dhati kwetu. #wemarchon”.