Raphael Tenthani
Katika maisha ya kawaida tumezoea kuona kuwa watangazaji na waandishi wa habari hupendelea kuonekana SMART kwani wao ni kioo cha jamii,,ila kwa hili ni tofauti>>>>>
Pichani ni Raphael Tenthani, mwakilishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) nchini Malawi.
Aina yake ya mavazi na uvaaji wake umezua gumzo katika mitandao jamii. Ralph amezoeleka kuonekana katika mavazi ya 'hovyo hovyo', yaliyolowa, machakavu na yaliyotoboka huku viatu vikiwa vimeachama, nywele 'vululu vululu' na sura ya 'kilevi'.
Mwandishi huyu wa habari hujihudhurisha alivyo katika kazi zake mbalimbali za kuhojiana na kurusha habari bila kujali ustaarabu wa eneo husika hata ikiwa ni kwenye zulia jekundu.
Wengi wanasema mkosoaji huyu mkubwa wa Serikalizote zilizoongozwa na Marais ndugu, Bingu (marehemu) na Peter Mutharika, huenda anafanya hivyo ili kutimiza masharti ya 'mganga' aliyemsaidia kupata ujasiri,akili nyingi na kazi katika shirika kubwa la utangazaji la BBC. Wanadai ikiwa atakiuka masharti hayo, huenda akapoteza kazi yake na kuwa 'juha'.
Vyovyote viwavyo, Raphael "Ralph" Tenthani bado ni mwakilishi wa BBC nchini