SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 10 Septemba 2016

T media news

MSANII RAYVANNY ASEMA SNURA MAJANGA NI CHANGAMOTO KWAKE

Baada ya kutoka video ya “Natafuta Kiki” pamekuwa na zengwe, kwa kile kilichoonekana kuwa ni mahaba juu ya Snura na Rayvanny kwa lile denda zito lililopigwa kitandani.Akipiga stori na eNewz Rayvanny amesema “Ni kweli ile scene ya kitandani ilinipa wakati mgumu sana, hasa ukizingatia ile shepu ya Snura, kuna wakati nilisahau kama tuko location”.Lakini kwa upande wa Snura anasema yeye aliifanya ile scene kama kazi tu, kama ambavyo script ilimtaka afanye ndicho alichokifanya, na wala hakumtamani Ray.
Snura kwa ujasiri akaongeza kwa kusema “Kama script inataka nimkiss hata mwanangu ninaweza kufanya hivyo”.Lakini pia kwa upande mwingine Ray alipoulizwa juu ya sababu za kutumia video aliyojishut na Wema katika birthday ya Romy Jones, alisema “Sina tatizo kabisa na Wema na tokea zamani nilitamani sana Wema aonekane kwenye hii video yangu, lakini ilishindikana kumpata sababu ya u-bize wake hivyo nikaona bora nitumie tu ile video tukiwa kwenye birthday ya Romy Jones”.