SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 18 Septemba 2016

T media news

MOURINHO AJIWEKEA REKODI MPYA EPL, MAN UNITED IKIFUNGWA 3-1 NA WATFORD


Manchester United chini ya Jose Mourinho imepokea kipigo kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kushuhudia ikifungwa mabao 3-1 dhidi ya Watford, mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa kunako Uwanja wa Vicarage Road maskani kwa Watford.

Wafford walikuwa wa kwanza kupata bao kwenye dakika ya 34 lililofungwa na kiungo mshambuliaji wao Etienne Capoue.

Dakika ya 62 mshambuliaji kinda wa Man United Marcus Rashford alisawazisha bao baada ya mabeki wa Watford kushindwa kuokoa kichwa alichopiga na mpira kumrudia tena na kuukwamisha mpira wavuni.

Waford walipata bao la pili kupitia kwa mshambulaiji wao aliyetokea benchi Juan Camilo Zuniga mnamo dakika ya 84 na kuwachanganya kabisa United.

Wakiwa bado wanajiuliza namna gani ya kusawazisha na pengine kuongeza bao, United walijikuta wakiruhusu bao la tatu lililofungwa na Troy Deeney kwa mkwaju wa penati dakika ya 90 baada ya Fellaini kumchezea madhambi Zuniga.

Hii imekuwa ni mara ya kwanza kwa Mourinho kupoteza michezo mitatu mfululizo ya ligi kwenye msimu tangu ilivyotokea Februari 2002, wakati huo akiwa meneja wa Porto.

Dondoo muhimu za mchezo

Capoue amefunga magoli manne kutokana na mashuti matno yaliyolenga lango kwenye msimu huu wa Premier League.Rashford amefunga magoli mengi kwenye michuano yote kwa Manchester United zaidi ya mchezaji yeyote tangu alipoacheza mchezo wake wa kwanza kabisa mwezi Februari. Amefunga mabao 10.Goli la Zuniga ni goli la mapema kufungwa na mchezaji aliyetokea benchi tangu mara ya mwisho mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi kufanya hivyo (sekunde ya 37) dhidi ya Aston Villa mwezi Februari.Tangu alipocheza mchezo wake wa kwanza Agosti 2014, Daryl Janmaat amepiga pasi nyingi za magoli zaidi ya mchezaji yeyote kwenye Premier League (11).Manchester United wamefunga goli lao la 800 la ugenini kwenye Premier League, 96 zaidi ya timu yoyote England.