SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 6 Septemba 2016

T media news

Hoja za Lissu zatupiliwa mbali na Mahakamani

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeitupilia mbali hoja ya Mawakili wa Tundu Lissu ya Kumtaka Camilius Wambura Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar ea Salaam (ZCO)mahakamani hapo kama shahidi,anaandika Faki Sosi.

Akitoa uamuzi huo Yohana Yongolo Hakimu Mkazi Katika Mahakama hiyo amesema kuwa hakuna ulazima wa shahidi huyo kutokana na muda upande  wa utetezi kuleta mashahidi mahakamani hapo haujafika.

Katika  kesi hiyo  Lissu anatuhumiwa kutoa maneno ya uchochezi kwa kumuita Rais John Magufuli kuwa ni ‘dikteta Uchwara’.

Lissu anadaiwa kutamka maneno hayo mara baada ya kutoka mahakamani katika kesi nyingine inayomkabili ya kutoa maneno ya uchochezi kupitia gazeti la MAWIO.

Awali tarehe 25 Septemba Wakili wa Serikali Bernard Kongola aliieleza mahakama kuwa walikuwa na mashahidi wawili ambao aliwataja kuwa ni Mratibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Kimweli na Staff Sajenti Ndege.

Hata hivyo kabla ya kesi hiyo kusikilizwa, kiongozi wa jopo la mawakili wa Lissu, Peter Kibatala aliiomba mahakama wapewe maelezo ya mlalamikaji katika kesi hiyo kabla ya kufanya jambo lolote, jambo ambalo liliibua mvutano wa hoja baada ya kupingwa na upande wa mashtaka.

Wakili Kongola aliieleza mahakama kuwa mlalamikaji katika kesi hiyo ambaye ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, si miongoni mwa mashahidi wao wanaokusudia kuwaita mahakamani.

Pia alisema kuwa kwa mujibu wa sheria hawalazimiki kutoa maelezo hayo ya mlalamikaji kwa mtu ambaye si shahidi.

Akijibu hoja hizo, Wakili Kibatala alidai kuwa taarifa ya huyo mlalamikaji ndio chanzo au iliyosababisha kesi hiyo na kwamba iwapo watamleta au hawatamleta lakini maelezo yake ni sehemu ya kesi hiyo.

Alidai kuwa hata mashtaka yaliyopo chini ya sheria ya magazeti ni ya muhimu na kwamba hawawezi kujitetea bila kuyaona na kwamba hata kama upande wa mashtaka hautamuita, wao wataiomba mahakama aitwe kwa lazima.

Hivyo aliiomba mahakama iulazimishe upande wa mashtaka uwapatie maelezo hayo ya mlalamikaji.
Kesi Hiyo itaendelea kusikilizwa tarehe 5 Oktoba Mwaka huu, ambazo Jamhuri itaendelea kutoka ushahidi Mahakamani hapo.