Olivier Giroud bado haelewi sababu hasa ya kwanini baadhi ya mashabiki wa Ufaransa ambao ni vipenzi wa Karim Benzema ambaye ameenguliwa kwenye timu hiyo walichagua kumzomea wakati wa Michuano ya Euro mwaka huu.
Mshambuliaji huyo wa Arsenal aliifungia Ufaransa mabao matatu kuelekea hatua ya fainali, huku Benzema akiwa hayupo kwenye kikosi hicho kutokana na kuwa katika uchunguzi juu ya sakata lake la picha za utupu na mchezaji mwenza Mathieu Valbuena
Sauti kutoka baadhi ya sehemu za uwanjani zilisikika zikimzomea Giroud hali ambayo haikuwa ikimfurahisha kutokana na kuamini kutostahili kufanyiwa vitendo hivyo.
“Nilikuja kugundua kwamba watu waliokuwa wakinizomea hawakuwa wale wasio nipenda bali ni wale ambao wanampenda Benzema,” alisema.
“Sijui kwanini waliamua kufanya vile. Niltoka kwenye ligi nikiwa na msimu mzuri kabisa na Arsenal. Kiukweli sikujisikia vizuri kwa walichokifanya.”
Giroud alifunga goli moja katika ushindi wa mabao 3-1 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Italy.
He has 21 goals from 56 caps for Les Bleus.
Mpaka sasa amefunga mabao 21 kwenye michezo 56 aliyocheza kwenye taifa hilo.