Clouds FM imemkwapua mchekeshaji aliyegeuka kuwa mtangazaji wa EFM, Kicheko na aliyekuwa nyota wa kipindi cha Singeli ‘Genge.’
Kicheko ambaye kabla ya kwenda EFM alikuwa member wa Ze Comedy ya EATV, aligeuka kuwa lulu ya EFM kwa utangazaji wake wenye vituko vingi.
Kicheko (Katikati)
Kuchukuliwa na Clouds FM kunakuwa pigo kubwa kwa EFM.
“MUNGU.. NIMETIMBA @cloudsfmtz NA WEWE TIMBA….RAIS WA USWAZI KAA TAYARI… MSHAMBA KAELEWA,”
ameandika Kicheko kwenye picha aliyoiweka Instagram ikionesha sehemu ya mapokezi ya Clouds Media.
Mchekeshaji huyo ataanzisha kipindi kiitwacho ‘Uswazi Flava’ hapo Clouds FM. Hivi karibuni Clouds wameonesha kuupa pia kipaumbele muziki wa Singeli ambao EFM imechangia kwa kiasi kikubwa kuutangaza.
Singeli sasa imezalisha mastaa kama Man Fongo na Sholo Mwamba.