SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 1 Agosti 2016

T media news

TIMU ZINAZOSHIRIKI LIGI KUU (VPL)KUKABIDHIWA VIFAA ALHAMISI



Timu ambazo zitashiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara(VPL)zitakabidhiwa vifaa mbalimbali kwa ajili ya msimu mpya wa 2016/17 Alhamis ya wiki hii katika hafla fupi itakaofanyika LAPF tower Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Akiongea na gazeti hili, Matina Nkurlu Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ndiyo wadhamini wakuu wa ligi, alisema kuwa zoezi la kukabidhi vifaa vya michezo kwa msimu ujao utakaotimua vumbi mwezi huu tarehe 20 lipo tayari kabisa na litafanyika tarehe 4 siku ya alhamis .

Alivitaja vifaa vitakavyokabidhiwa kuwa ni jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, mipira,soksi, vilinda ugoko, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vifaa vingine vingi vinavyohitajika,vyote kwa pamoja kwa mujibu wa mkataba.

“Vifaa vyote kwa ajili ya ligi ya msimu ujao vipo tayari kilichobakia ni kuvikabidhi siku ya alhamis ili timu ziweze kuendelea na maandalizi mengine kabla ya ligi kuanza mwishoni mwa mwezi August”.Alisema Nkurlu.

Alisema hafla hiyo ya kukabidhi vifaa inatajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa Chama Cha Soka,Viongozi wa klabu mbalimbali vinavyoshiriki katika ligi,wachezaji kutoka timu mbalimbali bila kusahau wadau wengine wa soka.

Visit website