SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 2 Agosti 2016

T media news

NAY WA MITEGOA AMALIZANA NA BASATA,ATOA KAULI


 Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) lilitoa tamko la kuufungia wimbo wa msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego uitwao ‘pale kati‘ kwa kigezo cha kutokuwa wa madili lakini pia BASATA walitangaza kumfungia Nay kutoshiriki kazi yoyote ya kisanii.
Sasa Agosti 2, 2016 staa huyo amepatikana kwenye Exclusive  kayaongea haya >>> ‘Mimi na basata tumeshamalizana kuanzia sasa hivi watu waendee tu ku-request wimbo unaendelea kupigwa media zote mimi na basata tumeyamaliza, wimbo una version mbili na video nne tofauti’
‘Video ya kwanza itaanza kutoka wiki ijayo, version ya pili ya audio ya ‘pale kati’ ndio ina marekebisho ambayo yalifanywa kutokana na maagizo ya BASATA, wimbo huu hautakuwa na utofauti sana na ule wa mwanzo ila maneno machache tu nimebadili kama walivyotaka‘ – Nay