Kiungo wa Mtibwa Sugar Ibrahim Rajab ‘Jeba’ amesema ni wakati wake sasa kuitumikia timu ya taifa baada ya kusubiri kwa muda mrefu kuitwa kwenye kikosi cha Stars.
Jeba ameitwa kwa mara ya kwanza kwenye timu ya taifa baada ya kocha wa timu hiyo kutaha kikosi cha wachezaji 24 watakaoingia kambini mwishoni mwa mweji Julai kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Nigeria.
“Namshukuru Mungu kwa kuweza kuitwa timu ya taifanahisi huu ni wakati wangu nitafanya kazi na nitajitahidi ili nifikie malengo niliyojiwekea,” alisema Jeba wakati akifanyiwa mahojiano na Azam TV.
“Kila kitu kinawakati wake, wakati wangu ulikuwa bado, nahisi huu ni wakati wangu ndiyo maana mwalimu kaniita.”
Jeba alianzia soka lake kwenye kituo cha kukuzia vijana cha Azam FC, msimu uliopita alionesha kiwango cha juu akiwa na klabu yake ya Mtibwa Sugar na kuisaidia kucheza fainali ya Mapinduzi Cup kabla ya kuisaidia kumaliza katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligu kuu Tanzania bara.