wnyekiti wa TLP, Agustin Mrema akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya wananchi wa Zanzibar kudumisha umoja wao na kuachana na kufuata kauli za baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaochochea vurugu leo jijini Dar es Salaam.
MMwnyekiti wa TLP, Agustin Mrema akitoka ukumbi wa mikuutano marabadaa ya kumaliza mkutano huu ulio fanyika leo jijini Dar es Salaam
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
CHAMA cha Tanzania Labour Party (TLP) kimetaka wananchi wa Zanzibar kudumisha umoja wao na kuachana na kufuata kauli za baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaochochea vurugu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa TLP, Agustin Mrema amesema kuwa kauli za viongozi wa siasa visiwani humo zinachochea kuvuruga amani hivyo wanatakiwa kupuuza.
Amesema hakuna mtu aliye juu ya sheria hivyo kuwepo kwa watu wanaochochea kuvuruga waangaliwe kama wahaini na hatua zichukuliwe dhidi yao katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama.
Mrema amesema kuwa hata nchi wahisani waache kuingilia mambo yetu ya ndani kutokana wao hawaishi huku na hata mauaji yakitokea hawaguswi kwa lolote.
Aidha amesema kuwa amani ikivurugika Zanzibar hata Tanzania bara haiwezi kuwa salama hivyo kauli za kuvuruga amani lazima ziangaliwe katika kulinda masilahi ya wananchi wa pande zote mbili.
Mrema amesema viongozi wachukue hatua dhidi ya watu wanaochochea vurugu za kisiasa kwa masilahi yao binafsi ya kutaka kuchukua madaraka nguvu kwa kuwaandamanisha wananchi.
Hata hivyo amesema kuwa Zanzibar ina historia ya mwaka 2001 ya kuuawa watu kutokana na vurugu za kisiasa hivyo lazima kwa sasa suala la uchochezi liangaliwe macho mawili dhidi ya watu wanaotaka kuvuruga amani katika mazingira hayo.
Amesema mahakama ya ICC haingalii viongozi wa serikali na hata viongozi wa kisiasa ambao kwa namna moja wanakuwa wamehusika katika kusababisha mauaji kutokana na kauli wanazozitoa.