SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 6 Aprili 2016

T media news

Vanessa Mdee analipwa kila muziki wake unapochezwa kwenye Radio na TV yoyote South Africa

Kwenye dunia ya sasa Wasanii wa muziki pia wanayo nafasi ya kulipwa au kujiingizia pesa kutokana na vyanzo mbalimbali na hiyo yote ni kutokana na muziki wao ndio maana sio kitu kigeni tena kuona msanii analipwa pale nyimbo zake zinapochezwa redioni.

Kama ulikua hujui, mwimbaji staa wa Tanzania Vanessa Mdee huwa anapokea pesa zake mara kwa mara kutokana na nyimbo zake kuchezwa kwenye Radio na TV za Afrika Kusini ambapo hii imekua ni kanuni inayofatwa kwa baadhi ya nchi, Radio na TV kuwalipa wasanii kutokana na jinsi nyimbo zao zilivyochezwa.

Sio kila msanii anaweza kulipwa kama hivyo, kwa Wasanii wanaotoka nje ya nchi kuna vigezo vinatazamwa kukuwezesha kusajiliwa na mamlaka husika na baada ya hapo unakua kwenye mzunguko wa kulipwa kama Wasanii wengine wa nchi hiyo wanavyolipwa.

Vanessa anasema ‘Kwanini Tanzania tusiende juu zaidi? ni kitu kizuri sana hiki…… kuanzia nilipotoa wimbo wa no body but me niliofanya na rapper K.O wa South Africa ndio nimeanza kulipwa sababu nilikua sijajiandikisha kabla ya hapo, South Africa msanii yeyote mziki wake ukichezwa kwenye Radio, TV au migahawani na sehemu nyingine analipwa‘

Sijajua kwa Uganda lakini Kenya kumekua na hii sheria kwa muda sasa hivi na nilikwenda wakati flani nikaambiwa mpaka Taxi, Saluni, Baa na sehemu nyingine za public kama club za usiku na hotelini wamiliki wake hulazimika kulipia ada ya kila mwaka na kupewa stika maalum kuwaruhusu kucheza muziki wa Kenya ambapo Diamond Platnumz wa Tanzania hulipwa kila mwezi maana ni miongoni mwa wasanii wa nje ya Kenya waliojisajili kwenye mamlaka inayosimamia malipo hayo.