SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 6 Aprili 2016

T media news

Aliyempachika Muna Love Ujauzito ni Kizungumkuti..Petit Man Ajing'ata ng'ata

Muna Love akiwa na Kalala Junior
Hali imezidi kuwa tete baada ya kuvuma kwa tetesi kuwa anayetajwa kama mke wa Kalala Junior mwanadada Muna Love ametundikwa mimba na Petit Man.

eNewz ilifanya mahojiano na Muna Love na alisema kuwa "Sina mimba ila nimeshiba tu". Lakini kutokana na muonekano wa tumbo lake kuwa kubwa fununu ziliendelea kuwa Muna ana ujauzito wa Petit Man.

Petit Man alipohojiwa na eNewz alijing'ata ng'ata kutoa maelezo ya kutosha na kusema "Acha watu waendelee kuhisi tu wanavyovihisi" huku akikataa kukanusha tuhuma hizo moja kwa moja au kuzikubali.

eNewz ilimtafuta Kalala Junior ambaye naye pia alisuasua kutolea maelezo juu ya mzozo huo, huku pia akikataa kuwa mume wa Muna Love na kusema kuwa Muna na yeye walikuwa ni wachumba tu!
Bado sekeseke hili halijapata majibu ya kueleweka kutokana na wahusika wote kupiga chenga kutoa majibu yanayofafanua ukweli wote.