SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 19 Machi 2016

T media news

wachambuzi wanasema inaonekana bado hakuna ufanisi katika ushirikiano kati ya makundi ya Boko Haram na IS

Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau ambae alitangaza kulitii kundi la Dola la Kiiislamu miezi kumi na mbili iliyopita lakini wachambuzi wanasema inaonekana bado hakuna ufanisi katika ushirikiano kati ya makundi hayo mawili.

Wakati kundi la Boko Haram lilipotangaza kulitii kundi la Dola la Kiislamu IS nchini Iraq na Syria mwaka jana, kulikuwa na hofu ya uasi wa umwagaji damu kaskazini mashariki mwa Nigeria ungetokea kwa kiwango kikubwa, kwa kuwa makundi hayo ya kigaidi yalikuwa yameungana rasmi.

Kufuatia tangazo la kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau kulizuka hofu na wasiwasi kwamba wapiganaji wa kigeni wangemiminika katika mataifa yanayolizunguka ziwa Chad na kuuchochea mzozo ambao awali ulikuwa wa kikanda.

Kundi la Boko Haram linaonekana kuwa dhaifu na limesambaratika baada ya operesheni ya kijeshi dhidi yake iliyodumu mwaka mmoja. Shekau amesikika mara mbili tu tangu alipotoa ujumbe wa sauti Machi 2, 2015 akiahidi kumtii kiongozi wa kundi la Dola la Kiislamu, Abu Bakar al-Baghdadi.