SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 23 Machi 2016

T media news

Diamond Platnumz Ukishindana na Juma Nature Jukwaa Moja Utaaibika


Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu msanii mkongwe wa Bongofleva Juma Nature kufunguka kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) na kusema kuwa anahitaji shoo moja tu uwanja wa taifa ambayo itamkutanisha yeye na msanii ambaye kwa sasa anasumbua kwenye Bongofleva Diamond Platnumz ili kuona nani ni mkali kati yao.

Mashabiki kwenye ukurasa wa Facebook wa (EATV) walifunguka mambo mengi na wapo watu ambao wanamuunga mkono Juma Nature wakisema kuwa Diamond Platnumz hatauweza muziki wa Juma Nature stejini huku wengine wakisema kuwa Juma Nature kwa Diamond Platnumz bado sana, mvutano wenyewe ulikuwa kama hivi:-

"Diamond ataaibika sana siku akipanda jukwaani kupambana na Sir Juma Nature, asijekubali suala hilo, maana yeye (Diamond) hata awe na Dancers wake, Nature akiwa peke yake tu anatosha kuwaamsha watu, tena uwanja wa taifa pale ndio hata asithubutu," aliandika Harrison Haroun Makaye.

"Kujaza uwanja na kushangiliwa na mashabiki haikusaidii kitu nyanyuka ushindane kimataifa, kweli unajua kuimba ila tatizo Diamond haimbi muziki kwa kushindana na mtu. Na wala hajawai kutangaza kuwa yeye ndio anajua kuimba," hii ni kwa mujibu wa Phemmy Mkuyawa
"Diamond nyimbo zake ni za kuwaburudisha na kuwafurahisha masisita du, lakini mzee mzima Juma Nature mistari yake inasomeka na inakubalika kwa watu wote na rika zote na haina powder wala nini," Fine Jerry naye alifunguka hivyo.

"Ha ha ha ha bado haijaniingia hiyo. Juma Nature na Diamond wapi na wapi? labda angesema tumpambanishe yeye Juma Nature na wasanii kama kina Chege au Temba hao! ndiyo type yake, ila King Kiba ndiye apambane na Dangote siyo yeye mimi hilo sijaafikiria kabisa," Joyce Jackson aliposti mawazo yake hayo.

"Wajinga wajinga ndiyo watasema Diamond mkali kuliko Nature msiangalie visenti au video au kaimba na wasanii wa Nigeria, swali nani mkali kwa kuimba, Diamond mjanja wa kusaka hela na mishe anaziweza ila kwa kuimba hata Ali Kiba anamzidi. halafu Nature kuimba ni nature yake sio anaekti," Rabi Intocavel naye alitupia hiyo.

Hizo ni baadhi ya Comments za watu kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa (EATV) ambapo mashabiki bado wanaendelea kuvutana wengine wakisema Juma Nature atamkalisha chini Diamond Platnumz kama shoo hiyo itakuja kufanyika huku wengine wakisema kuwa Diamond Platnumz si wa kushindana na Juma Natute wakiwa na maana kuwa lazima atamshinda Juma Nature.