SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 24 Juni 2017

T media news

HEBU LEO TUJIKUMBUSHE MUVI YA SARAFINA MUVI BORA ZAIDI YA MUDA WOTE KUWAHI KUTOKEA BARANI AFRIKA.



Muvi ya SARAFINA ni moja ya muvi au sinema maarufu sana Afrika na Dunia nzima iliyoigizwa mwaka 1992 kwa ushrikiano wa waigizaji wa marekani (Hollywood) na wale wa Afrika Kusini iliyokua na lengo la kuonesha jinsi ambavyo sera ya ubaguzi wa makaburu dhidi ya Waafrika na Wazawa wa Afrika kusini ilivyokuwa ikiendelea na ilivyokuwa ikiwaathiri watu wa Afrika ya kusini kipindi kile.

Muvi hii ililenga zaidi mauaji ya halaiki ya wanafunzi wa SOWETO ya nchini Afrika Kusini waliokuwa wanapingana na unyanyasaji wa Makaburu hao.

Kama ulishafatilia au kuangalia muvi hii utagundua kuwa Mhusika mkuu katika muvi ile alikuwa anaitwa SARAFINA ambaye aliigiza kama mwanafunzi wa kike aliyekuwa akiwaongoza wanafunzi wenzake kupinga ubaguzi na uovu uliokuwa ukifanywa na viongozi wa makaburu dhidi ya wananchi weusi na wazawa wa Afrika Kusini wakati ule.

HEBU pia tuupitie wasifu wa muhusika mkuu katika hii muvi huyu Sarafina mwenyewe sasa ambaye jina lake halisi anaitwa LELETI KHUMALO.

Leleti Khumalo alizaliwa mwaka 1970, ni mwigizaji wa Ki-Zulu wa Afrika Kusini aliyejipatia umaarufu  kutokana na nafasi yake ya kuongoza kama Mhusika mkuu katika filamu ya SARAFINA, na katika filamu zingine kama vile HOTEL RWANDA, YESTERDAY na INVISCUS.

Leleti Khumaro alimaaarufu kama SARAFINA alizaliwa katika kitongoji cha Mashu, kaskazini mwa Durban, nchini Afrika Kusini.
Leleti Khumalo (SARAFINA) alionyesha nia ya kuigiza akiwa katika umri mdogo sana, alijiunga na kundi la vijana la kuchekesha  liitwalo AMAJIKA, lililoongozwa na TU NOKWE.

Mwaka 1985 alijaribu kuimba muziki akiwa na Mtayarishaji na Mwigizaji maarufu wa Afrika Kusini MBONGENI NGEMA ambapo wimbo alioimba ulikuwa na kuwa wa kimataifa ambao ulijulikana kama  SARAFINA. NGEMA ndiye aliyeandika sehemu kubwa ya wimbo huo ulioitwa SARAFINA kwa Leleti Khumalo . Huyu bwana NGEMA ndiye mwanaume ambaye baadae alimuoa SARAFINA.

Mwaka 1992, SARAFINA  alishirikiana sambamba na Mwana mama muigizaji kutoka Mareka aitwaye WHOOPI GOLDBERG (amabaye ndiye aliyekuwa mwalimu wa akina sarafina katika somo la historia katika muvi ile, na alijulikana kama MRS. MARY MASOMBUKA). Pia alishirikiana na magwiji MIRIAM MAKEBA na JOHN KANI katika filamu iliyotengenezwa chini ya kampuni ya DARELL JAMES ROOTD , filamu iliyoitwa ”SARAFINA!”, ambayo ilisambazwa duniani kote, na ikawa filamu kubwa zaidi na zaidi kuwahi kutolewa barani Afrika.

LELETI KHUMALO baadae alichaguliwa kuwania tuzo za IMAGE pamoja na waigizaji wenzake; Angela Bassett, Whoopi Goldberg na Janet Jackson.

Katika upande mwingine, mwaka 2015  alikaribishwa katika visiwa vya Zanzibar, Tanzania, kama mgeni rasmi wa sherehe maarufu filamu za kiafrika ambapo waandaaji wa sherehe hiyo walikuwa wakiadhimisha miaka 18 ya shrehe hizo  zinazojulikana kama ZANZIBAR FILM FESTIVALS.

Hivi sasa SARAFINA ni Muigizaji na Muongozaji wa
FILAMU ALIZOIGIZA

Miongoni mwa filamu ambazo mwanamama huyu aliwahi kuigiza ni;

Uzalo (2015 -)Winnie Mandela (2011)Invictus (2009) …. MaryFaith’s Corner (2005) …. FaithHotel Rwanda (2004) …. FedensYesterday (2004) …YesterdayCry, the Beloved Country (1995) (as Leleti Kumalo) KatieSarafina! (1992) …. SarafinaVoices of Sarafina! (1988).

#HEBU TUAMBIE UNAKUWA NA MTAZAMO GANI KUTOKANA NA MAUDHUI YA HII MUVI.