SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 7 Machi 2017

T media news

Jicho la 3: Tatizo la Msuva ni kukosa penati?


Na Baraka Mbolembole

Tatizo la Saimon Msuva si kukosa penalti, tatizo kwake ni kuichezea klabu kubwa zaidi nchini Tanzania.

Msuva amekuwa akikosolewa sana na mashabiki wa klabu yake. Si yeye tu, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, na sasa mashabiki wa Yanga wamehamia hadi kwa mlinzi wa kati Mtogo, Vicent Bossou na mshambulizi Mzimbabwe, Donald Ngoma.

Najiuliza mara kwa mara ni kwanini mashabiki wa Yanga wanasahau mapema msaada uliotolewa/unaoendelea kutolewa na wachezaji hao katika timu yao!

Chanzo cha mashabiki wa Yanga kumzomea mara kwa mara Msuva na kumkosoa Niyonzima ni kwasababu ‘wanaamini’ wachezaji hao ‘wana mapenzi na mahasimu wao Simba SC.

Msuva ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa miongoni mwa wachezaji wa Yanga, ana akili sana pindi unapomweleza jambo ndio maana ninaamini baadhi ya mashabiki wa klabu yake wanakosea sana wanapomtuhumu mchezaji ambaye alifunga magoli 17 na kushinda tuzo binafsi ya mfungaji bora katika ligi kuu Tanzania bara misimu miwili iliyopita.

Wanakosea zaidi wanamtuhumu kucheza chini ya kiwango wakati tayari amehusika kikamilifu katika magoli zaidi ya 20 ya timu katika ligi inayoendelea hivi sasa. Tangu alipoingia katika timu hiyo akiwa kinda wa U19 hadi sasa bila shaka kiungo huyo mshambulizi wa pembeni amefanya jitihada kubwa na ataendelea kufanya vizuri kutokana na utulivu wake.