Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kuanzia usiku wa jana Machi 1, 2018 hadi leo Machi 2, 2018 kutakuwa na vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi ya nyanda za Juu Kaskazini Mashariki.
Taarifa ya TMA iliyotolewa imebainisha maeneo hayo kuwa ni mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro ambapo mvua hizo itazidi milimita 50 ndani ya saa 24 huku ilieleza hali hiyo inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua.
TMA imewashauriwa wakazi wa maeneo husika kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zinazotolewa.