Nchi ya Nigeria inakisiwa kuwa taifa lenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika ambapo inaelezwa lina zaidi ya watu milioni 170.
Wakati ikielezwa kuwa uchumi wa Nigeria umeporomoka sehemu kubwa baada ya kuanguka kwa bei ya mafuta duniani. Leo January 03 2016 BBC wameripoti kuwa Serikali ya Nigeria imeanza kutekeleza mpango mpya wa kuwapa fedha za kila mwezi, watu milioni moja maskini na wasiojiweza katika jamii.
Hatua ya kwanza ya kutolewa kwa mshahara huo, ambapo kila mtu atapokea dola 16 kwa mwezi sawa na Tsh 34,923, imeanza katika majimbo tisa kati ya majimbo 16 nchini Nigeria