SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 23 Desemba 2016

T media news

CCM kimewatimua wenyeviti wawili

Chama cha Mapinduzi mkoani Rukwa kimewafukuza uanachama wenyeviti wa serikali za vijiji wawili kutokana na mienendo ya wenyeviti hao kuwa kinyume na Katiba ya CCM na usaliti na kufuta adhabu kwa wanachama waliokuwa wamepewa na CCM ngazi za wilaya.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM mkoa wa Rukwa, Clemence Bakuli ameeleza hayo katika kikao na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ngazi ya mkoa mjini Sumbawanga.

Kutokana na maamuzi hayo wenyeviti hao wa vijiji wanapoteza sifa ya kuwa wenyeviti wa Serikali za Vijiji wanavyoongoza kwa mujibu wa sheria inayowataka viongozi wa kisiasa katika ngazi mbalimbali kuwa na udhamini wa chama cha siasa.

Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Sumbawanga Mjini Selemani Kilindu amefukuzwa rasmi uanachama wa CCM baada ya kujiuzuru wadhifa huo na kuanza kutenda kinyume na katiba ya CCM.