SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 23 Desemba 2016

T media news

African Lyon kiboko ya vigogo VPL

African Lyon imeendelea kuvipa shida vigogo vya VPL, baada ya Yanga kutoka nyuma kusawazisha goli na kuambulia pointi moja katika matokeo ya 1-1.

Lyon walitangulia kupata bao kupitia kwa Ludovick lakini Tambwe alisawazisha bao hilo kuiokoa timu yake isipoteze mchezo.

Bado Yanga wamekuwa wababe mbele ya Lyon kwa sababu katika michezo nane iliyopia Lyon hawajafanikiwa kutoka na ushindi, wamepata sare mbili sawa na pointi mbili huku Yanga wao wakiwa wameshinda mara sita na sare mbili na kupata pointi 20 dhidi ya Lyon.

Mchezo uliopita uliochezwa August 28 mwaka huu, Yanga iliifunga Lyon 3-0 magoli yakifungwa na Deus Kaseke, Simon Msuva na Juma Mahadhi.

Lyon imekuwa tishio kwa vigogo kwasababu iliweza kuizuia Azam katika mchezo wa ufunguzi wa msimu huu 2016/17 na kutoka sare ya kufungana bao 1-1 huku Azam wakitoka nyuma na kusawazisha.

Simba walijikuta wakichezea kichapo cha goli 1-0 November 6 mwaka huu mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru ikiwa ni raundi ya kwanza ya msimu huu.

Lyon wakawabana tena Azam katika mchezo wa marudiano raundi ya pili ya ligi na kutoka suluhu December 18, 2016 kabla ya Yanga kulazimisha sare katika mchezo wa leo December 23.

African Lyon imefanikiwa kupata pointi 6 dhidi ya Yanga, Simba na Azam. Tayari imesha cheza mechi mbili na Azam na Yanga huku ikisubiri mechi moja ya marudiano dhidi ya Simba.

Mechi za African Lyon vs Azam, Yanga na Simba

20/08/2016 Azam 1-1 African Lyon

18/12/2016 African Lyon 0-0 Azam

28/08/2016 Yanga 3-0 African Lyon

23/12/2016 African Lyon 1-1 Yanga

06/11/2016 African Lyon 1-0 Simba

Yanga inaendelea kusalia katika nafasi ya pili ikiwa na pointi zake 37 pointi moja nyuma ya Simba ambayo itacheza kesho December 24 dhidi ya JKT Ruvu. Endapo Simba itashinda mchezo huo itaongeza gap la pointi hadi kuwa nne kwa sababu itakuwa imefikisha pointi 41 huku Yanga ikiwa na pointi 37, lakini kama Simba itafungwa bado itaendelea kuongoza kwa pointi moja wakati ikitoka sare itakuwa kileleni kwa pointi mbili.