SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 30 Septemba 2016

T media news

Uchambuzi na dondoo uelekea Oktoba 1 Yanga vs Simba


“Si siku ya kukosa kabisa nchi itakuwa kwenye matukio mawili ya kihistoria lile la upandaji miti kisha tunaelekea pale taifa kwenye “Dar Derby” ni mechi ya watani wa jadi Yanga vs Simba, tunaanza kudondoa ndogondogo kuelekea mtanange huo.

MSIMAMO:                                            

YANGA:  Tayari wamejikusanyia pointi 10, Wakishinda michezo mitatu, kufungwa mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mmoja, ikiwa na magoli manane ya kufungwa na moja la kufungwa hivyo GD ni magoli 7, ikiwa nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi.  (Yanga ina mchezo mmoja mkononi)

SIMBA: Hawa ndio vinara wa ligi, Mara baada ya kucheza mechi sita na kujikusanyia pointi 16, ikishinda mechi 5 na kutoka sare mchezo 1. Ikifunga magoli 12 na kufungwa mawili. GD ni 10.   “Timu zote mbili zinaonekana ni nzuri kwenye ukabaji na ushambuliaji (offensive & defensive).

UHASAMA:                                             

YANGA: Wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Stand United, pia kumbu kumbu ya kujizolea point I zote 6 kutoka kwa mahasimu wenzao simba msimu uliopita.

SIMBA: Itaingia na kumbukumbu ya kushinda mchezo 5 kati ya sita msimu huu huku ikiwa timu ikiyofunga magoli mengi zaidi 12 ikiwa ipo juu kwenye ‘Goal difference’ yaani 10, pia kumbukumbu ya kupoteza pointi zote sita msimu uliopita kwa Yanga.

MIFUMO: (KIMBINU ZAIDI)                

YANGA: (4-4-2)                          

Yanga inatumia mfumo wa 4-4-2 yaani ikiwa na mabeki wanne nyuma juma Abduli, Dante, Bossou, Ngwali na viungo wanne yaani Msuva, Twite (Niyonzima, Ngonyani), Kamusoko, Kaseke (Mahadhi) washambuliaji wawili Ngoma na Tambwe.

Mfumo huu Mara nyingine huwa unabadilika pindi Yanga inaposhambulia hii ni kutokana na udhaifu wa Yanga upande wa kushoto (beki wa kushoto), hii inaifanya Yanga kutumia zaidi upande wa kulia ndio maana kati ya magoli nane waliyofunga Yanga msimu huu yalitokea upande wa kulia, ukiacha ile penati iliyokoswa na kumaliziwa kwenye mechi dhidi ya Majimaji, hivyo hucheza(3-1-4-2) muda mwingi wakishambulia ingawaje si muda wote, yaani Dante ,Bossou, Ngwali hutengeneza ‘situational three backs’, mbele yao akicheza  Mbuyu Twite kama kiungo mkabaji (hufanya ‘back up’ kwa Juma Abduli wanaposhambuliwa).

Juma Abduli hucheza juu zaidi kwenye (kiungo) winga ili kusaidia mashambulizi huku Simon Msuva akifanya movements kwenye wings na half spaces, kutokana na kuvunjwa kwa upande wa kushoto wakati wa kushambulia.

Kaseke husogea kwenye half space na muda mwingine huingia katikati kusaidia kiungo kumiliki mpira, ndio maana goli la kwanza msimu huu lililofungwa na kaseke alifunga akitokea kati baada ya kupokea pasi kutoka upande wa kulia kwa Msuva, Kamusoko anacheza katikati kama muunganishi wa timu, Ngoma na Tambwe wanashambulia (mfumo hurudi kwenye 4-4-2 wanaposhambuliwa), Kamusoko ndiye anatechezesha timu akichukua mipira kutoka kwa mabeki wa kati wa Yanga na kuisambaza.

SIMBA: (4-4-2)                                      

Simba nao hutumia mfumo wa 4-4-2 tofauti operation tu Yaani mabeki wanne; Bokungu, Mwanjali, Lufunga, Mohammed Hussein (Tshabalala), kiungo: Kichuya, Mkude, Muzamiru, Mnyate, washambuliaji; Ajibu na Mavugo.

Mabeki wa kati wa SIMBA wanaonekana kutengeneza uwelewano mzuri yaani Method Mwanjali na Juko Murshid, mabeki wa pembeni ni wazuri ingawaje Tshabalala ni mzuri kwa kushambulia kuliko Bokungu, bado anaonekana mzito.

Nahodha Jonas Mkude anacheza kama kiungo mkabaji kazi yake ni kuchukua mipira na kuisambaza kutoka kwa mabeki wa kati wa timu hiyo, wakati wa kukaba hucheza kati ya mistari miwili yaani mstari wa mabeki na viungo, huku viungo watatu wa mbele yake wakitengeneza narrow formation ili kutengeneza compactness.

Kutokana na hii narrowing washambuliaji wa simba huangalia movement ya mipira kama ni kulia, aliyeupande huo (mara nyingi ni Mavugo) hushuka hadi kwenye half space muda mwengine hadi kwenye wing na kucheza kama “false inside forward” ili kupokea mpira kwenye upande huo na lengo ni “ku-stretch” ukuta wa timu pinzani kwani anapofanya hivyo beki wa kati wa timu pinzani humfuata na kuacha nafasi kubwa kati ya beki mmoja wa kati na mwengine hivyo  mshambuliaji mwengine hukimbia kwenye hiyo space kati ya mabeki  wawili (baada ya stretching) kuelekea kwenye boksi.

Mfano goli la kwanza la dhidi ya  Maji maji, Mavugo alipokea pasi kutoka kwa Kichuya akiwa kwenye wing Ajib alipiga shuti lililotemwa na mlinda mlango na kumaliziwa na Mnyate, pia goli la kusawazisha dhidi ya Ruvu Shooting ,Mavugo alisogea juu kuja kuchukua mpira na beki wa kati wa Ruvu Shooting hivyo kuacha space ambapo Ajibu alikimbia kwenye space hiyo krosi ya Tshabalala ilimkuta akiwa unmarked na kufunga.

Mipira mingi iliyopigwa na Simba kwenye kumi na nane ya timu  pinzani ilipigwa Simba ikiwa na mshambuliaji mmoja tu wa kati ndani ya boksi la timu pinzani, Mara baada ya mshanbuliaji mwingine kufanya ‘stretching’. Ndio maana goli la nne la Simba dhidi ya Majimaji Kichuya alikimbia kwenye open space katikati baada ya mabeki wa kati kufanyiwa stretching.

Ndio maana pamoja na kuwa na washambuliaji hatari, Simba bado viungo washambuliaji wanaongoza kwa magoli kazi yao ni kukimbia kwnye space baada ya stretching.

UDHAIFU NA UMAKINI                          

YANGA

Yanga wanaonekana kuwa wadhaifu upande wa kushoto kwa Haji Mwinyi Ngwali, upande ambao atacheza na Kichuya na huyu ni hatari lazima wawe makini.

Yanga wanaonekana kutomudu ‘pressing game’ mfano mechi dhidi ya Stand, Yanga wanaonekana pia kukosa plan B inapofeli plan A.Yanga lazima wawe makini na stretching plan ya washambuliaji wa Simba hivyo Mbuyu Twite atatakiwa kucheza kama sweeper    ili kuziba space baina ya believe mmoja wa kati na mwengine, pindi washambuluaji wa Simba wanapofanya stretching Yanga wawe makini na movement za Mkude kwani huyu hupokea mipira na kuisambaza kwingine yaani huanzisha mashambulizi.

SIMBA

SIMBA wanapokaba pindi timu pinzani inapocheza kati hutengeneza narrowing na kuacha wings opens kwa ushambuliaji wa timu ya Yanga wa kutumia wings hasa Msuva  na  Juma Abduli inaweza kuwagharinu hii kutokana na ubunifu wa Kamusoko.

Pia Simba wawe makini na movement za Kamusoko kwani huyu ndie anayechezesha timu. Mabeki wa kati wa Simba  wawe makini na Tambwe na Ngoma kwani ni hatari sana kwa mipira ya vichwa na goli mmoja kati ya mawili wakiyofungwa simba  msimu huu lilifungwa kwa kichwa dhidi ya Ndanda.

MWISHO

Timu zote zina nafasi ya kushinda mchezo huu umakini na utumiaji mzuri wa nafasi utaamua matokeo. Mechi hii ni ngeni kwa Mwanjali ,Mavugo, Bokungu, Dante,Chirwa na wengineo.